Tajudeen Abdul-Raheem (6 Januari 1961 – 25 Mei 2009) alikuwa mwanazuoni na mwanaharakati wa Afrika. Kazi yake kuu ilikuwa kama katibu mkuu wa baraza la saba la kongamano la Pan-Afrika mwaka 1994. Pia aliwahi kuwa mkurugenzi wa haki Afrika, naibu mkurugenzi wa kampeni ya milenia ya umoja wa mataifa kwa Afrika, pamoja na mwandishi wa magazeti na majarida kote Afrika.[1]